Hon.Bashe Posts

Filter Events

Nimehudhuria mkutano muhimu wa wadau wa kilimo Dodoma

Leo, nimehudhuria mkutano muhimu wa wadau wa kilimo Dodoma, katika Ukumbi wa Mabeho, ambapo tumekuja pamoja kujadili Sera ya Maendeleo ya Benki 2024 na Sera ya Taifa ya Bima 2024. Mkutano huu umegusia haja ya kuwa na sera za moja kwa moja zinazohusiana na mitaji, ugharamiaji, na bima katika sekta za uzalishaji kama kilimo, mifugo, na uvuvi.
April 18, 2024

Kongamano la Mwaka la Kujadili Mageuzi ya Sera za Mifumo ya Chakula, Uvuvi na Mitugo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) leo Aprili 17, 2024 amekuwa geni rasmi kwenye ufunguzi wa Kongamano la Mwaka la Kujadili Mageuzi ya Sera za Mifumo ya Chakula, Uvuvi na Mitugo.
April 18, 2024

MKUTANO WA 14 WA WADAU WA KAHAWA NCHINI.

Leo nimehudhuria Mkutano Mkuu wa 14 wa Wadau wa zao la Kahawa kujadili namna ya kuboresha na kukuza zao hili la kimkakati nchini. Mkutano huu umewakutanisha Wakulima, Wazalishaji, viongozi wa vyama vya ushirika pamoja na wamiliki wa viwanda vya uchakataji wa zao la kahawa.
April 17, 2024

Nashukuru jana nilipata nafasi ya kujibu maswali wakati wa Mkutano wa Bunge wa 15 wa Bunge la 12.

Nilipata nafasi ya kuongelea masuala kadhaa yakiwemo 1. Kukamilika kwa Upembuzi Yakinifu wa hekta 67,000 wa Bonde la Mto Rufiji 2. Zao la Mahindi – Serikali itaendelea kununua mahindi kupitia NFRA na tuko kwenye hatua za mwisho za majadiliano na Nchi za Zambia, Mozambique na Namibia kununua mahindi yetu.
April 16, 2024

Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Tasnia ya Tumbaku Kitaifa

Leo nimefungua na kuongoza Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Tasnia ya Tumbaku Kitaifa, tarehe 28 Machi 2024 katika Hoteli ya Morena, Dodoma.
April 4, 2024

Leo nimefungua Mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Chai 2024 katika Hoteli ya Morena, jijini Dodoma.

Mpango wa serikali ya awamu ya Sita ni kukabiliana na changamoto mbalimbali, ikiwemo kuimarisha sheria ya wakulima wadogo ili walipwe kwa wakati; kuwezesha Ujenzi wa viwanda 5 vya kusindika chai na viwili vya kuchanganya chai (kiwanda kimoja kila mwaka); kuwezesha mifumo ya umwagiliaji katika Mkoa wa Njombe hekta zaidi ya 500; na kuwezesha wakulima wadogo kuchakata chai na kuuza kwenye Mnada moja kwa moja.
March 27, 2024

GET IN TOUCH

Office ya Mbunge

Follow Bashe on Social Media